Matthew 1

Kumbukumbu Za Ukoo Wa Isa Al-Masihi

(Luka 3:23-38)

1 aHabari za ukoo wa Isa Al-Masihi mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu:


2 bIbrahimu akamzaa Isaka,
Isaka akamzaa Yakobo,
Yakobo akawazaa Yuda na ndugu zake,

3 cYuda akawazaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari,
Peresi akamzaa Hesroni,
Hesroni akamzaa Aramu,

4 Aramu akamzaa Aminadabu,
Aminadabu akamzaa Nashoni,
Nashoni akamzaa Salmoni,

5 dSalmoni akamzaa Boazi, na mama yake Boazi alikuwa Rahabu,
Boazi akamzaa Obedi, ambaye mama yake alikuwa Ruthu,
Obedi akamzaa Yese,

6 eYese akamzaa Daudi ambaye alikuwa mfalme.

Daudi akamzaa Sulemani, ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria.

7 fSulemani akamzaa Rehoboamu,
Rehoboamu akamzaa Abiya,
Abiya akamzaa Asa,

8 Asa akamzaa Yehoshafati,
Yehoshafati akamzaa Yoramu,
Yoramu ndiye Yehoramu, maana yake ni Yehova yu juu.

Yoramu akamzaa Uzia,

9 Uzia akamzaa Yothamu,
Yothamu akamzaa Ahazi,
Ahazi akamzaa Hezekia,

10 hHezekia akamzaa Manase,
Manase akamzaa Amoni,
Amoni akamzaa Yosia,

11 iwakati wa uhamisho wa Babeli, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake.


12 jBaada ya uhamisho wa Babeli:
Yekonia alimzaa Shealtieli,
Shealtieli akamzaa Zerubabeli,

13 Zerubabeli akamzaa Abiudi,
Abiudi akamzaa Eliakimu,
Eliakimu akamzaa Azori,

14 Azori akamzaa Sadoki,
Sadoki akamzaa Akimu,
Akimu akamzaa Eliudi,

15 Eliudi akamzaa Eleazari,
Eleazari akamzaa Matani,
Matani akamzaa Yakobo,

16 knaye Yakobo akamzaa Yusufu ambaye alikuwa mumewe Mariamu, mama yake Isa, aitwaye Al-Masihi.
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.

17Hivyo, kulikuwepo na jumla ya vizazi kumi na vinne tangu Ibrahimu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi hadi wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli, na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli hadi Al-Masihi.

Kuzaliwa Kwa Isa Al-Masihi

(Luka 2:1-7)

18 mBasi Kuzaliwa kwake Isa Al-Masihi kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alikuwa ameposwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Mariamu alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19 nKwa kuwa Yusufu, mwanaume aliyekuwa amemposa alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Mariamu hadharani, aliazimu kumwacha kwa siri.

20 oLakini mara alipoazimu kufanya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto na kusema, “Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21 pNaye atamzaa mwana, nawe utamwita Jina lake Isa,
Isa ni Iesous kwa Kiyunani, na kwa Kiebrania ni Yoshua au Yeshua. Maana yake ni Yehova ni wokovu.
kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.”

22 rHaya yote yalitukia ili litimie lile Bwana alilokuwa amenena kupitia nabii, akisema: 23 s“Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita Jina lake Imanueli”: maana yake, “Mungu pamoja nasi.”

24 tYusufu alipoamka kutoka usingizini, akafanya kama vile alivyoagizwa na malaika wa Bwana, akamchukua Mariamu kuwa mke wake. 25 uLakini hawakukutana kimwili mpaka Mariamu alipojifungua mwanawe kifungua mimba akamwita Jina lake Isa.
Copyright information for SwhKC